Wednesday 24 February 2010

WASIOONA WALALAMIKA

Mwanachama wa chama cha wasioona (ZANAB) Sabra Nassor amesema serikali haiwatendei mema katika kudumisha demokrasia yao ya uchaguzi kwa vile hakuna karatasi maalum za kupigiwa kura kwa watu wa aina hiyo.
Malalamiko hayo aliyatoa jana huko katika ukumbi wa Pemba clove in Tibirinzi chake chake wakati alipokuwa atika mkutano wa majadiliano kuhusu dhima na wajibu wa vyombo vya habari katika kuleta umoja na mshikamano katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa.
amesema hivi sasa ni muda mrefu toka kufanyika kwa uchaguzi lakini inawezekana watu wa aina hiyo kuwatumia watu wengine kwa ajili ya kuwapigia kura wakati hawana uhakika kwamba matakwa yao ya uchaguzi yanatekelezwa.
aliendelea kusema kuwa wao kama wananchi wa nchi hii hawana uhakika na kuchaguliwa lakini kuendelea kwa tatizo hilo ni kuwanyima fursa muhimu kwa kutumia watu wengine.

No comments:

Post a Comment